MICHEZO
Kufuatia shutuma za Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Gerald Darmanin, kuwa Karim Benzema “ana uhusiano ” na kundi la kigaidi la Muslims Brotherhood, seneta wa Ufaransa Valerie Boyer ,ameibuka na kutoa kauli tata dhidi ya Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid.
Kupitia taarifa kwenye vyombo vya habari, Seneta huyo ametaka hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya Benzema, ikiwa tuhuma za kujihusisha na kundi la “Muslims Brotherhood ” zitathibitishwa kutoka kwa Waziri huyo wa mambo ya ndani.
Kwenye taarifa hiyo ,Seneta Boyer alisema,
“Kama kauli za Waziri wa Mambo ya Ndani ni kweli, lazima Karim Benzema awekewe vikwazo “.
“Kwanza Benzema apokonywe tuzo yake ya Ballon dOr,lakini pia,ni lazima mchezaji huyo avuliwe uraia wa Ufaransa. Hatuwezi kukubali Mfaransa mwenye uraia pacha ,na kujulikana kimataifa, atuvunjie heshima na kuisaliti nchi kiasi hiki”.
Mjjadala na tuhuma hizo imeibuka baada ya Benzema kukaa kimya kwenye shambulizi la kigaidi lililohusisha mauaji ya mwalimu Ufaransa nje ya mji kidogo wa Paris, huku siku chache baada ya tukio hilo,Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa pole kwa raia wa Palestine huku akitaka haki itendeke.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.