SAMIA MGUU SAWA KUELEKEA 2025

0:00

NYOTA WETU

Rais Samia Suluhu Hassan ameibuka tishio kwa vyama vya upinzani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa 2025 kutokana na umati mkubwa anaovuta kwenye ziara zake akiwa kwenye mikoa mbalimbali.

Popote aendako kwenye ziara zake kwenye mikoa mbalimbali, Rais Samia amekuwa akilakiwa na umati mkubwa wa watu jambo ambalo sasa ni nyota ya kijani kwake kuelekea Uchaguzi wa 2025 anaweza kuibuka kidedea mapema.

Kada mbalimbali za wananchi,ikiwemo ya vijana madereva bodaboda ,kina mama lishe, wakulima ,wavuvi,wafugaji ,wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kumlaki Rais ,kitu ambacho akikuwahi kutokea.

Ingawa bado ni mapema mno na Rais Samia bado hajatangaza nia yake ya kugombea urais 2025, lakini ni wazi Rais Samia kwasasa anaonekana ni mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi kwasasa nchini na ni turufu kubwa ya uchaguzi mkuu.

Katika ziara zake za hivi karibuni kwenye mikoa ya kusini na katikati mwa nchi amejizolea maelfu ya watu hasa mkoa wa Singida ambayo ilionekana ni ngome ya Lissu lakini imekuwa tofauti kwani amepata watu wengi .

https://youtu.be/hL-BB3dbpag?si=yYVNeYM50cKOh1Vp

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

RAIS LUIS RUBIALES KUFUNGWA JELA KWA KOSA...
MICHEZO Waendesha mashtaka nchini Uhispania wametaka aliyekuwa Rais wa Shirikisho...
Read more
ALIYEMUUA MTOTO KISA KUMRUSHIA JIWE AKIOGA KUNYONGWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
WHY MARRIAGE IS NOT A COMPETITION
Stop competing with your spouse who earns more and who...
Read more
THE BENEFITS OF SEX WHEN YOU DO...
Gets you to start the day right. Morning glory has...
Read more
Raila Explains Reasons for Calling for Dialogue,...
Raila Odinga, the leader of the Azimio la Umoja -...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ya kiongozi bora wa mwaka 2023 katika Tuzo za Kiongozi Bora wa Afrika kwa Mwaka 2023 (African Leadership Person of the Year) kama Kiongozi Bora wa Mwaka katika Amani na Usalama barani Afrika.

Leave a Reply