ZIARA YA MFALME KENYA YAIBUA MAZITO

0:00

HABARI KUU.

Wazee wa jamii ya Nandi nchini Kenya wametoa wito kwa kurudisha fuvu la Koitalel Arap Samoei ,chifu pamoja na kiongozi wa kiroho na kijeshi aliyeuawa na Waingereza mwaka 1905.

Matakwa hayo mapya yanakuja siku chache kabla ya ziara ya mfalme Charles III nchini Kenya Oktoba 30,2023.

Samoei aliyeongoza upinzani mkali dhidi ya wakoloni ,aliuawa na mwanajeshi wa Uingereza kanali Richard Meirnertzehagen ,baada ya kuwalaghai Samoei na Viongozi wengine wa Nandi wa kuhudhuria mkutano wa mapatano.

Kulingana na gazeti la Daily Nation la nchini Kenya, wazee hao pia wanataka kurejeshwa kwa vitu vyao vya kitamaduni vilivyoibwa na kufidiwa kwa ukatili waliofanyiwa jamii wakati wa utawala wa wakoloni .ikiwa ni pamoja na mauaji ,kuwekwa kizuizini na kuwahamisha watu wa jamii ya Nandi kwa nguvu.

Fuvu la Koitalel Arap Samoei inasadikika kuwa katika mkusanyiko wa makumbusho mahali fulani nchini Uingereza.

Wazee wa Nandi mara kwa mara wamekuwa wakiomba kurejeshwa kwa mabaki hayo ya Samuel.

“Tunamsihi Mfalme Charles, tunahitaji kupata fuvu hilo lirudishwe Nandi tufanye mazishi ya heshima.

David Samoei aliliambia shirika la utangazaji la KTN mapema mwaka huu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Businessman Wanjigi Granted Court Protection from Arrest...
The High court in Nairobi Issued a court order on...
Read more
Kwanini CAF Imemtoza Samuel Eto'o faini...
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limemtoza faini ya Dola...
Read more
SIRI YA MICHAEL JACKSON YAFICHUKA ...
NYOTA WETU Michael Jackson aliundiwa mfumo wa kucheza ambao ulipingana na...
Read more
MFAHAMU OSMAN BEY KIPENZI CHA WAPENDA FILAMU...
NYOTA WETU
See also  MAHAKAMA YATOA AMRI MWILI KUFUKULIWA NA KUZIKWA UPYA
Burack Ozcivit wengi mnamfahamu kama Osman Bey kama...
Read more
"WHY WE AWARDED BOBRISKY BEST DRESSED FEMALE"...
OUR STAR 🌟 A Nigerian actress and filmmaker, Eniola Ajao,...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply