NYOTA WETU
Lionel Messi azawadiwa Pete nane za dhahabu kuwakilisha tuzo zake nane za Ballon d’Or baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo,siku ya jumatatu.
Mshambuliaji huyo wa Inter Miami, alipewa Pete hizo za dhahabu na kampuni ya mavazi na vifaa vya michezo ya Adidas. Inaripotiwa kuwa pete hizo nane zenye maandishi ya kuonyesha matukio muhimu ya Messi zitapigwa mnada.
Moja ya pete hizo ina nyota tatu kuashuria ushindi wa kombe la Dunia kwa timu ya Taifa ya Argentina, pia nyingine itakuwa na na namba “91” kuonyesha idadi ya mabao ambayo ni rekodi kwa Messi ya kufunga idadi kubwa ya mabao kwenye msimu mmoja wa 2012 .
Vilevile, moja kati ya picha iliotumiwa na Adidas, inamuonyesha Messi akiwa ameweka mikono yake usoni ,akiwa amevalia pete hizo nane ,ikiwa ni njia ya kumuenzi nguli wa kikapu (NBA) ,Bill Russell aliyepiga picha sawa na hiyo,mnamo mwaka 1996.