NYOTA WETU.
Mahakama imesema Asamoah Gyan (37) amlipe fidia aliyekuwa mke wake nyumba 2,moja ikiwa nchini Uingereza na nyingine ikiwa Accra, Ghana,pia ampe kituo cha mafuta cha petroli na gari 2.
Ni baada ya vipimo vya DNA kubaini kweli yeye ndiye baba halisi wa wanawe 3 aliokuwa akiwatilia mashaka kuwa sio wake kwa madai aliyekuwa mke wake alichepuka.
Gyan ambaye kabla ya kustaafu soka mwaka huu aliwahi kuwa Nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa Ghana 🇬🇭 “black stars” na pia kucheza vilabu kadhaa ikiwepo Sunderland ya nchini Uingereza, yeye ndio alitaka ndoa yao iliofungwa mwaka 2013 ivunjwe .
Nyumba ya Accra, Ghana aliyopewa mke wake huyo wa zamani ilinunuliwa kabla au kuelekea walipotaka kufunga ndoa yao mwaka 2013.
Pia ,Mahakama imetoa amri kwa Asamoah kutoa pesa za matumizi kwaajili ya wanawe hao watatu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 5 yaani £ 1,729 kwa kila mwezi.
Mahakama imeeleza mama wa watoto hao watatu anayejulikana kwa jina la Gift hakuwa na mchango wa moja kwa moja wa kipesa kwa mali za mumewe,isipokuwa yeye ndiye alikuwa muangalizi na mlezi wa watoto hao watatu na hivyo mwanasoka huyo kwa upande wake yeye alipata muda mzuri wa kujiimarisha kisoka na kuchan7a kiuchumi huku mkewe akiwa anapambana na watoto pekee yake.