SABABU ZA MASHABIKI KUWATUPIA PESA WACHEZAJI WA NEWCASTLE

0:00

MASTORI

Mechi kati ya Borussia Dortmund na Newcastle, usiku wa jumanne ililazimika kusimama kwa muda baada ya mashabiki wa Dortmund kurusha dhahabu feki na mifuko bandia uwanjani, huku wakibeba bango linalosomeka kwa maneno “HAMJALI KUHUSU SOKA- MNACHOTHAMINI NI PESA TU”.

Kitendo hicho cha mashabiki wa Borussia Dortmund kilitafsiriwa kimakosa,huenda kililenga wamiliki wa Newcastle kutoka Saudia Arabia, lakini ni wazi mashabiki walipanga kupinga mipango ya UEFA kutaka kutambulisha mfumo mpya kwenye Ligi ya Mabingwa kuanzia msimu wa 2024-25.

Mfumo huo mpya utashuhudia ongezeko la idadi ya timu zitakazoshiriki katika hatua ya makundi kupanda kutoka 32 mpaka 36 ,ikiwa ni mfumo unaolenga kunufaisha ligi kubwa Ulaya kama Premier league ambayo kwa mfumo huo inaweza kuingiza vilabu vitano.

Vilevile, baada ya kuwepo makundi nane yenye timu nne ,mfumo mpya utahusisha ligi moja kubwa ycnye timu 36.

Kila timu itacheza dhidi ya timu 10 tofauti, ikiwa ni michezo mitano nyumbani na mitano ugenini. Timu 8 bora zitafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora ,huku timu zitakazomaliza kuanzia nafasi ya 9 mpaka 24 zikichuana kwenye mtoano ili kujihakikishia nafasi ya kutinga nafasi ya 16 bora .

Kuanzia hapo utaratibu utakuwa kama ilivyozoeleka na timu zitachuana mpaka zitakapo salia timu mbili zitakazocheza fainali.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WAKATOLIKI WAZUIWA KUJIUNGA FREEMASON ...
HABARI KUU Waraka mpya uliotiwa saini na Papa Francis, umesema mafundisho...
Read more
The wife of footballer Kayode Olanrewaju publicly...
Olanrewaju Kayode’s wife, Dora, has firmly refuted any claims that...
Read more
IGNORE THE RUMOURS ZACK ORJI IS ALIVE
OUR STAR 🌟
See also  Dembele keeps getting better, says PSG boss Luis Enrique
Nollywood veteran actor, Zack Orji is alive!...
Read more
Nationwide Public Participation Reveals Strong Opposition to...
A recent report from the National Assembly indicates that the...
Read more
"DOING MUSIC WAS NOT MY DREAM I...
Nigerian artist Zlatan Ibile has disclosed that he fell into...
Read more

Leave a Reply