WATU WANNE WAKAMATWA SAKATA LA UTEKAJI

0:00

MICHEZO

Watu wanne wameripotiwa kukamatwa baada ya sakata la Wazazi wa Mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz kutekwa.

Watu hao wanashtakiwa kwa kuteka na kuiba ,na wanatarajiwa kupelekwa Mahakamani leo katika mji mmoja ujulikanao kama Riohacha uliopo Kaskazini mwa Colombia.

Mmoja wa watu hao aliyetambulika kama Yerdinson Bolivar anatajwa kuwahi kuwa kocha Kwenye shule ya soka ya baba yake mzazi Luis huko Barrancas.

Mamlaka nchini Colombia zinamtuhumu Bolivar kwa kuomba kazi ili Kuwa karibu na kuweza kumchunguza mzee Diaz.

Picha kadhaa zimeonekana jinsi mtu huyo alivyokuwa akimfatilia mzee huyo mara kwa mara mpaka madukani.

Wengine waliokamatwa ni pamoja na madereva wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki wakati wa zoezi la utekaji.

Mamlaka nchini Colombia zinataka haki itendeke juu ya kutekwa huko ambako kundi la kihalifu la ELN lililohusika limesema wazi kuwa lilifanya makosa.

Kutekwa kwa raia nchini Colombia limekuwa jambo la kawaida likiwa linaongozwa na makundi ya kihalifu. Mazungumzo ya amani yamekuwa yakiendelea kati ya kundi hilo na Serikali ya Colombia tangu Machi 2020.

Kundi hilo lilitangaza kuacha utekaji hata hivyo limeendelea kuwateka watu wasio na hatia na kutoa madai ya fidia kubwa hili kuwaachia.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HUYU NDIYE MREMBO ZAIDI DUNIANI 2023 ...
NYOTA WETU. Mrembo wa nchini Nicaragua 🇳🇮 Sheynnis Palacios Cornejo...
Read more
Enzo Fernandez aomba Radhi kwa Ubaguzi Michezoni
Klabu ya Chelsea imeingia kwenye sintofahamu baada ya kiungo Enzo...
Read more
Sababu ANDREW KAMANGA kukamatwa
MICHEZO Rais wa chama cha Soka Zambia Andrew Kamanga amekamatwa...
Read more
HAALAND APEWA ADHABU KWA KUKASHIFU
MICHEZO
See also  RUBEN AMORIM AKANA UVUMI WA KUJIUNGA NA LIVERPOOL
Mchezaji wa Manchester City, Erling Haaland huenda akaadhibiwa...
Read more
WANAUME WENYE MIAKA 50 WAONGOZA KUWA WAATHIRIKA...
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imebainisha kuwa WANAUME wenye...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply