0:00
MICHEZO.
Viongozi wa klabu ya Maniema Fc ya DRC wamesema viongozi wa Simba SC waliwafata na kuwaahidi ofa nono ili wamsajili , Max Nzengeli.
Hii imetokea baada ya siku za hivi karibuni mchambuzi, Jemedari Said kufichua kuwa ,Max Nzengeli yupo ndani ya klabu ya Yanga kwa mkopo . Viongozi wa Simba SC waliamini na kufanya mawasiliano na klabu ya Maniema Fc ili kumsajili nyota huyo.
Kiongozi wa klabu ya Maniema Fc ambaye akupenda kujitambulisha amesema;-
“Ni kweli Simba SC wametufuata na kutupa ofa wakimtaka Max Nzengeli, tumewaambia Max Nzengeli ni mali ya Yanga na biashara yoyote ya mauzo ya Max ipo kwenye mikono ya yanga . Ni mchezaji wao.
Tulimuuza Max Yanga japo tuliweka kipengele kwamba, Yanga wakimuuza kwenda klabu nyingine Maniema tutapata asilimia kadhaa ya mauzo”.
Related Posts 📫
Liverpool-born Ng has long held the desire to play for...
MICHEZO
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed...
MAKALA
Wanasayansi wanasema, hadi umri wa miaka 35, wanawake wengi...
CELEBRITIES
Mercy Johnson, a popular Nollywood actress, has hinted at...
The following is Rafa Nadal's retirement statement in which the...