MAKALA
Watafiti wa Marekani wanasema wamegundua ni kwanini baadhi ya watu hupata maumivu ya kichwa baada ya glasi moja ya mvinyo,lakini wakinywa vinywaji vingine vya vileo wanakuwa sawa.
Timu ya chuo kikuu California inasema ni kutokana na mchanganyiko wa vitu katika zabibu nyekundu ambavyo vinaweza kuharibu jinsi mwili unavyobadilisha Pombe.
Mchanganyiko huo ni antioxidants au flavanol inayoitwa quercetin.
Zabibu nyekundu hutengeneza zaidi quercetin zinapopigwa na jua.
Hii ina maana mvinyo mwekundu wa bei ghali , una madhara zaidi ya kusababisha maumivu ya kichwa.
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.