MICHEZO
Shirikisho la mpira wa miguu ( FIFA ) limeiondolea klabu ya Simba adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kuilipa klabu ya Teungueth ya Senegal.
Awali FIFA iliwafungia wekundu wa Msimbazi baada ya kushindwa kuilipa Teungueth kutokana na mauzo ya Sakho kufuatia wababe hao wa Senegal kufungua kesi FIFA ikidai malipo kutokana na malipo ya Sakho.
Simba ilishindwa kesi hiyo na kutakiwa kulipa malipo hayo ndani ya siku 45 tangu maamuzi yaliyofanywa na kamati za FIFA,lakini Simba SC ilishindwa kesi kwa kushindwa kulipa ndani ya muda husika.
Baada ya kukamilisha malipo hayo basi ni rasmi sasa hata Shirikisho la kandanda Tanzania (TFF) limeifungulia Simba kufanya usajili wa ndani.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.