HABARI KUU
Masheikh 9 miongoni mwa walioshikiliwa kwa zaidi ya miaka 10 katika gereza kuu la Kisongo wamesomewa mashtaka katika Mahakama kuu ya kanda, ambapo 6 kati yao wamekutwa na hatia ya kulipua Kanisa Katoliki la parokia ya Mtakatifu Joseph Olasiti mwaka 2013, hivyo kuhukumiwa kunyongwa.
Waliohukumiwa ni Imam Jaafar ,Hashima Lema,Yusuf Ali Huta, Hamadi Waziri, Abdul Hassa Masta, Kassim Idrissa, na Abashiri Hassan Omari na walioachiwa huru ni Abdul Humud Wagoba, Abdurahmani na Amani Musa Pakasi ( ambaye amerejeshwa gerezani kwa kesi nyingine).
Katika hukumu hiyo Jaji alionesha kuridhishwa na ushahidi wa polisi kwamba Masheikh hao akiwemo Imam Mkuu wa Masjid Quba,sheikh Jaafar Hashim Lema walilipua kanisa katoliki hilo na kusababisha madhara makubwa.