HABARI KUU
Joachim Marunda kwa jina maarufu “Master J” amefunguka kufuatia yanayoendelea huko Ulaya na Marekani kuhusu baadhi ya watu maarufu kukubwa sana na kesi za unyanyasaji wa kingono ambapo ameeleza kuwa :-
“Hivyo vitu vipo hadi kwetu ,naomba Mungu isije kufunguka ya Bongo hii ni mbaya,yaani bora ya nje kuliko Tanzania, kwanza hapa watoto wa kike waliopo kwenye tasnia wanateseka sana,naamini ipo siku wataongea”.
Kutokana na madai ya namna hii kuwa ni wengi hushtushwa zaidi pindi tuhuma hizo zinapofika mbali na kuzaa matunda kama ilivyokuwa kwa wanamziki wa R&B na Hip-hop kutoka Marekani. Robert Sylvester Kelly (R Kelly),kufungwa miaka 31 ,baada ya kukutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na watoto miaka ya nyuma.
Master J anaweka wazi kuwa jambo ili na Tanzania lipo,baadhi ya wasanii wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya ngono na kuwalipa ili waweke siri.
Master J ni Mtayarishaji wa mziki wa kizazi kipya akiwa ni mmiliki wa Bongo Records label 🏷 na jaji maarufu wa kutafuta vipaji vipya vya wanamziki maarufu kwa jina la Bongo Star Search (BSS).
yandanxvurulmus.SjyvW4v0OYAo