MAPENZI
1. Usijifanye unaumwa kwa lengo la kukataa kumpa mumeo tendo la ndoa. Mpe mumeo, tendo la Ndoa kwa mwanaume ni muhimu.
2. Usimkaripie mumeo kwani kufanya hivyo,hiyo ni ishara ya kumkosea adabu.
3. Usiseme mapungufu au madhaifu ya mumeo kwa ndugu au marafiki. Siku zote hayo huwa yanakurudia.
4. Usionyeshe hisia zako kama hasira kwa mumeo
5. Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine kwani kila mtu yuko tofauti na mwingine. Jinsi anavyokupenda au mwonekano wake usiupe mfanano na wengine ulio wajua kabla yake. Kufanya hivi kutakufanya upoteze upendo wako kwake. Msome kama kitabu kipya.
6. Usisahau kuwa huyo ni mumeo,huyo sio kijakazi wako. Timiza majukumu yako
7. Jukumu la kumlinda mumeo kwa gharama yoyote ni la kwako. Usiruhusu watu wakusaidie,watakusaidia visivyo.
8. Usimpe lawama mumeo anaporudi nyumbani hata kitu. Ni muda wa kumpa pole na kumpa motisha zaidi.
9. Jiepushe kuwa karibu na mazungumzo ya wanawake ambao hawako kwenye ndoa . Hawa wana mawazo hasi ,wanaweza kukupandikiza mawazo yao.
10. Usipende kumhukumu mumeo. Hakuna mwanaume anapenda kusumbuliwa.
11. Usiruhusu marafiki zako kujenga ukaribu muno na mumeo
12. Usimdharau au kuonyesha kumkosea adabu mumeo mbele ya watoto wenu. Wanaume sio wa kihivyo,anaweza kuvunja ndoa hii kikubwa aendelee kulinda na kutunza heshima yake.