HABARI KUU
Taasisi ya Thabo Mbeki imepinga vikali tetesi zilizovuma kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Afrika kusini ameaga Dunia.
Mapema Januari 3,2024 ya hivi leo kwenye mitandao ya kijamii kulifurika habari kuhusu kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ,Thabo Mbeki kufariki. Taasisi hiyo imesema Bwana Mbeki yuko salama.
“Tunaiomba jamii kutafuta habari kwenye vyombo vya habari vya kuaminika kuhusu habari za Mbeki.
Mbeki aliingia Madarakani mnamo mwaka 1999 na kuondoka 2008 . Anakumbukwa kwa namna alivyopambana na ubaguzi wa rangi nchini humo na kwenye ukuzaji wa uchumi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Matukio ya mara kwa mara ya kuzushiwa kifo kwa Rais huyu mstaafu yamekuwa na mwendelezo ,kwani mwaka 2021 iliripotiwa Bwana Mbeki amefariki kwa ugonjwa wa Covid 19 kabla ya taasisi yake kukanusha vikali.