MAPENZI
Uzuri haupo kwenye mwonekano wa nje bali uzuri upo ndani ya mtu mwenyewe yaani kimawazo,kifikra na kiakili.
Walio wengi upendelea kuona uzuri wa Mwanamke lakini badala ya uzuri,urembo ndio huwa unaonekana. Wanawake wengi nguvu yao ipo kwenye urembo badala ya uzuri.
SIFA ZA MWANAMKE MZURI
1. Mwanamke mzuri huwa ahudhurii kila shughuli au tukio
2. Mwanamke mzuri huwa hapigi chakula alichokula picha na kukirusha kwenye mitandao ya kijamii
3. Mwanamke mzuri huwa ajisifii ana pesa ngapi?
4. Mwanamke mzuri sio mmbeya au ambaye hana siri. Kusema kila kitu ni tabia tu za wasichana na sio Mwanamke
5. Mwanamke mzuri ni fundi wa kupika. Mwanamke anajua ,Mwanamke anayeolewa ni yule anaejua kupika chakula kitamu.
6. Mwanamke mzuri ni yule anajua walau hata kujitegemea kwa baadhi ya mambo kama kununua nguo zake nk na sio mtu wa kukopa
7. Mwanamke mzuri anajua kujitafutia pesa sio mvivu.
8. Mwanamke mzuri sio wa kumkubalia mwanaume yeyote ,haijalishi ana pesa kiasi gani
9. Wanaume wengi upendelea kutumia mtego wa pesa kuwanasa wanawake lakini Mwanamke mzuri ana hela ili asije kutumiwa na wanaume kwa mtego wa pesa.
10. Mwanamke mzuri sio wa kwenda kwa kila mwanaume, kufua au kuosha vyombo. Mwanamke mzuri ana mipaka ya Mambo hayo
11. Mwanamke mzuri ana hofu ya kweli ya MUNGU
12. Mwanamke mzuri sio wa kubishana au kuweka mashindano na watu