MAPENZI.
Utunzaji wa sehemu ya siri ya Mwanamke (uke) ni jambo la kuzingatia sana ili kuepuka maambukizi , na ni vizuri kumweleza mpenzi wako mnaojaamiana ili nae aelewe juu ya umuhimu wa kutunza uke.
MAMBO YA KUZINGATIA NI HAYA
1. EPUKA KUINGIZA VIDOLE KWENYE UKE.
Wakati wa mahaba,ni kama sehemu ya maisha ya wengi ya kutiana vidole. Lakini jambo la kujiuliza,je ni yupi huwa anakumbuka kunawa mikono? Kuna wapenzi wengine wana kucha ndefu,ambazo zimebeba mpaka uchafu ambazo zinaweza kubeba bakteria na kuwaingiza sehemu hiyo nyeti ya uke.
Hata wadada wengine wanajiingiza vidole wakati wa kujichua,jambo ambalo ni hatari kwao kwa afya ya uke.
2. EPUKA KUJAMIANA KINYUME NA MAUMBILE.
Sipo hapa kuzuia ila ni hatari kufanya mapenzi ya sehemu ya aja kubwa. Wengi wana imani wakitumia kondomu basi wataepuka maradhi lakini ukweli ni kwamba, unaponya kuingiza uume kwenye sehemu ya haja kubwa na kuingiza kwenye uke basi unaingiza bakteria ambao wataenda kuharibu uke.
3. MATUMIZI YA DAWA ZA KUKAZA UKE.
Baadhi ya wanawake wamejikuta kwenye wakati mgumu sana ,ambapo wanaume huwa wanawalazimisha kwenda kutafuta tiba ya kukaza uke. Wanaume wanaona uke kama umelegea sana na kukosa utamu,jambo hili uwafanya wanawake kutafuta dawa za kubana uke. Baadhi ya dawa zimeharibu mpaka maumbile ya uke na kushindwa tena kupitisha uume mpaka labda wafanyiwe upasuaji tena.
4. MATUMIZI MAZURI YA SEHEMU ZA KUJISAIDIA. Huenda ni mwanamke unaesafiri au kuwa kwenye sehemu zenye mikusanyiko ya watu. Unapokwenda ,zingatia sana usafi wa kwenye sehemu za vyoo kwasababu ni haraka sana kubeba bakteria kwenye sehemu za uke.
5. USAFI WA NGUO ZA NDANI.
Nguo za ndani ni vizuri kufuliwa vizuri na kuanikwa vizuri mpaka zikauke. Wakati upo kwenye siku zako ni vizuri kuweka utaratibu wa kubadili nguo za ndani ili kuepuka kubeba bakteria.
6. MATUMIZI SAHIHI YA PEDI.
Wazazi wengi huwa wanabana matumizi kwa kuendelea kuwavisha watoto pedi zile zile kwa kuhofia gharama. Pedi , ni moja ya chanzo cha watoto hasa wa kike kupata magonjwa kama UTI. Pedi ni vizuri zinapofika baada ya muda kubadilishwa na sio ruksa kwa matumizi ya baadae.
Kumbuka ,uke unapokuwa unatoa harufu au usaha ni kwasababu ya maambukizi kwahiyo ni wakati wa kupata matibabu kwaajili ya afya yako.