HABARI KUU.
Mamlaka inayohusika na mambo ya Afya ya nchini Rwanda 🇷🇼 imeamua kurudisha dawa za fangasi zilizotoka nchini Kenya kwasababu zilizoelezwa ni za kiusalama.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini Rwanda (RFDA) imewaagiza waagizaji kurudisha tembe zote za fluconazole milligrams 200 zinazotengenezwa na universal Corporation, kampuni ya Kenya.
Pia imetoa amri kwa wasambazaji wadogo na wenye vituo vya afya kuacha mara moja kusambaza dawa hizo na kuzirejesha walikozipata.
Sababu iliotajwa ya kusitisha matumizi ni kuwa mzalishaji wa tembe hizo amebadili rangi kutoka ile ya awali.
Kulingana na RFDA, vifurushi vinne vya jumla vya tembe za fluconazole milligrams 200 zilizoingizwa nchini humo zilibadilika rangi na kuwa nyeupe baada ya kukaa kwenye kabati kwa muda mfupi.
Mamlaka hiyo imesema kuwa pamoja na tembe hizo kubadika rangi tayari zilikuwa zimeingia kwenye mzunguko nchini Rwanda.