MAPENZI.
Mwanamke kumpata mwanaume wa ndoto yake huwa sio jambo la kawaida.
Hata baadhi ya wanandoa huwa ni vigumu kwa haraka kupendana kwa hatua za mwanzo wa mahusiano yao ,huwa wanaenda kwa muda n baadaye kujikuta wametumbukia kwenye mapenzi mpaka hata kufunga ndoa.
Ila kuna baadhi ambao huwa hawahitaji muda mrefu kuwa katika mahusiano na kufunga ndoa,huwa wanatumia tu muda mchache.
Kuna wanandoa ambao ,siku yao ya kwanza tu walipokutana na wenza wao walikiri kwamba wamewapata wenza wao wa maisha.
Upendo ndani ya ndoa hizi ni wa kweli pamoja na kwamba hawakuweka mizizi ya kufahamiana kwa kina. Sasa hizi ndizo hisia ,ambazo hutokea unapokuwa umekutana na mtu wa ndoto yako
1. Huwa unapata hisia zisizo za kawaida kwa huyo mtu na hata ukijizuia huwa ni ngumu.
2. Huwa unapata hisia za tofauti zinazokunyima utulivu.
Hii huwa inatokea sio kwa sababu ya kulazimishwa au kwa miujiza. Hisia hizi huwa zinawavuta nyote kwasababu hisia sio za kutengeneza ni hisia za kweli za mapenzi.
3. Mvuto wako kwake huwa unaongezeka kila siku.
Mwanaume wa ndoto yako ataendelea kukuona wewe mzuri kila siku Kadri mnavyoendelea tofauti na mwingine ambaye mvuto wako kwake unaweza kushuka. Hili huwa linaendelea hata kwako,kwani na wewe huwa unaendelea kumpenda Kadri ya siku zinavyosogea.
4. Unakuwa na ujasiri hata wa kulipambania penzi lako.
Baadhi ya wanandoa kwa nyakati za mwanzo wa ndoa yao huwa wanaogopa kukwazana na hata kupigana endapo wametofautiana. Ila ukiwa na mtu wa ndoto yako hata akikupiga ,bado utaendelea kumvumilia na kumpenda. Hii ndio nguvu ya mwanaume wa ndoto.
5. Unakuwa na uhakika kwamba unakubalika na kupendwa.
Huwezi kujisikia hauna thamani au hupendwi,ni kwasababu ndani ya nafsi yako umeridhika. Wakati mwingine hata asipokuonyesha,utakuwa tu na uhakika unakubalika na kupendwa.
6. Huwa unafarijika kwasababu ya kuwa na ndoto sawa.
Mwanaume wa ndoto yako huwa anakutia midadi pale tu ,kila unachomwambia na anachokwambia vinaendana. Ili ni moja ya jambo moja kubwa ambalo baadhi ya wanandoa ulikosa. Kila Mwanamke angetamani mawazo yake yasikilizwe na hata kupata majawabu lakini walio wengi huwa wanapuuzwa.
7. Uhuru wa kuzungumza.
Kila Mwanamke anapenda atoe yaliyopo Ndani ya moyo wake. Mwanamke akiwa na mwanamume wa ndoto yake huwa anafunguka sana na hafichi kilichomo ndani yake ,kwahiyo basi anakuwa huru .Mwanamume wake huyu,atamsikiliza hata kwa mambo yote ambayo hayana uzito.
8. Unakuwa na hisia za kuwa salama.
Kwa kila jambo lako kwenye mahusiano unakuwa huna mashaka kwasababu ya mume wa ndoto yako. Unapokuwa unatembea njia unajua ,Mume wako yupo na hata akitokea wa kukukwanza hisia zitamwendea Mume wako.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.