MAPENZI
1. Wazazi kulala kwenye vitanda tofauti au vyumba tofauti kwenye nyumba moja. Ni kitisho kwa watoto.
2.Wazazi kuongea kauli zisizofaa au kutukanana mbele ya watoto. Watoto watashindwa kuwaheshimu.
3. Mzazi kumpiga mwenzake mbele ya watoto . Mtoto wa kiume ataona ,ni kawaida kupiga Mwanamke na mtoto wa kike ataona wanaume ni watu makatili.
4. Kuwashambulia ,kutowaamini na kuwasengenya watoto. Hii itawafanya watoto kiakili kuhama kihisia na kimwili nyumbani.
5. Wazazi kuwa na ushindani ndani ya nyumba. Hii itawafanya watoto kuamini familia sio Muungano.
6. Mwanamke kutomheshimu mume wako. Hii itamfanya mtoto wa kiume kuamini kuwa ni lazima aishi kwa kujiami pindi akioa na mtoto wa kike ataona kuwa mume hapaswi kuheshimiwa, jambo ambalo sio sahihi.
7. Wazazi kuwa na muda mchache wa kukaa nyumbani. Hii itawafanya watoto kuamini hawapendwi .
8. Wazazi kununiana ndani ya nyumba au kila mtu kujifanya yuko tu na mambo yake. Hii inawavunja moyo watoto.
9. Wazazi kutowajali watoto. Hii itawafanya watoto kuamini kuwa hawapo kwenye sehemu salama.
10. Wazazi kupigana mbele ya watoto. Hii itawafanya watoto kuamini familia sio sehemu salama kwao.