HABARI KUU
Mwanzilishi wa Benki ya ACCESS Duniani, Herbert Wigwe (57) amefariki kwa ajali ya ndege,jijini California Marekani.
Benki ya ACCESS yenye makao makuu nchini Nigeria ina matawi yake Tanzania, Congo,Ghana,Kenya, Uganda, Nigeria, Rwanda,Gambia,Guinea, Cameroon, Sierra leone ,Msumbiji,Botswana, Afrika Kusini, Ufaransa, Zambia na Uingereza.
Katika ajali hiyo iliotokea Februari 10,2024 saa nne usiku, waliofariki ni pamoja na Mke wake na mtoto wake wa kiume pamoja na watu wengine watatu waliofariki kwa ajali ya Helicopter.
Wigwe ambaye ni mzaliwa wa Ibadan Nigeria, alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa ACCESS holding ambayo ni kampuni mama ya benki ya ACCESS.
Helicopter ya Wigwe ambaye pia ni mmiliki wa chuo kikuu cha Wigwe ,ilikuwa ikielekea Las Vegas kabla ya kuanguka kwenye mpaka kati ya Nevada na California.
Mamlaka za anga nchini Marekani zimethibitisha kuwa hakuna aliyenusurika kwenye ajali hiyo huku zikifuatilia chanzo cha ajali hiyo.
Naye Rais Bola Tinubu wa Nigeria akizungumzia msiba wa Wigwe ,amesema ni msiba mzito na pigo kwa Nigeria na Afrika kwa ujumla kwenye sekta ya fedha.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.