KWANINI VIJANA HAWAOI WALA KUOLEWA TANZANIA ?

0

0:00

MAPENZI

1. WOGA.

Vijana wengi wana woga wa kuoa na kuolewa. Wanakwepa majukumu yaliyopo kwenye ndoa. Kwa mfano kijana wa kiume ana hofia,je pesa za kumlisha au kumvisha Mwanamke atazitoa wapi hasa pale anapojiambia hana kipato cha kutosha?

Wengine, wana woga wa kihisia kwamba nikiolewa kila siku lazima nifanye nae mapenzi, kila siku nimwambie “nakupenda” au kumbusu mke au mume na kumuomba msamaha lakini pia wengine wanaogopa kuoa au kuolewa kwasababu ya yale waliosikia au kuona kwa jamaa au ndugu.

2. HAWAPENDI KUKOSA UHURU WALIOZOEA.

Wanawaza wakiwa kwenye ndoa watakosa kukutana na marafiki zao au kwenda popote pale wanapojisikia .

3. PESA / KIPATO.

Hapa yapo makundi mawili hasa kwa vijana wa kiume. Kundi la kwanza, ni vijana ambao wanaogopa kuoa kwasababu hawana hela za kulipia mahari na kugharamia shughuli za harusi na Kundi la pili, ni wale wenye mshahara na kazi zao tu nzuri lakini wanataka kwanza wawe mamilionea wenye magari na majumba na biashara kubwa kubwa.

4. KULA UJANA.

Hapa nina maana ya kuwa anatamani afanye mapenzi na kila binti au kijana na awe na idadi fulani ya watu ambao amelala nao . Kuoa au kuolewa hakumpi mwanya wa kufanya haya.

5. BADO WANATAFUTA.

Hapa tunazungumzia na wale ambao hata mtaa ukiwa na mabinti au vijana bado wanatafuta wakamilifu ambao hawana kasoro. Pia, wapo wanaofanya maombi ili MUNGU awape wenza lakini bado hawaelewi kama wamepewa kweli au la!

6. MAMBO YA KIROHO.

Kuna wanaoingia kwenye mahusiano ya dhati lakini baada ya muda mahusiano hayo yanafika mwisho hata bila ya wao kuelewa ni nini kimetokea? Hapa huenda kweli kuna roho za shetani zinafanya kazi hasa kwa yale uliowahi kutamkiwa au kufanya. Hapa, maombi na kufunga kunahitajika ili Mwenyezi MUNGU akutoe kwenye vifungo hivi.

7. MAISHA KABLA YA NDOA.

Kuna vijana na mabinti wameamua kuishi wote bila kuoana mpaka wanafika hatua ya kupata watoto,katika mazingira haya ni vigumu kufunga ndoa maana kila kitu wanakuwa wanakifanya kama wana ndoa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  16 ROLES YOU SHOULD PLAY AS A GOOD WIFE

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading