MAPENZI
1. MUNGU humpa maono ya kuingia kwenye ndoa na wewe
2.MUNGU ufunua mambo yanayokuhusu wewe kupitia kwake
3. Atakulisha chakula cha kiroho kupitia maombi na Maandiko
4. Kupitia maombi yake kwa MUNGU, hakuna adui atakayekudhuru
5. Maombi yake kwa MUNGU ni kinga kwako kwenye Ulimwengu wa roho.
6. Itakuwa rahisi kwenu kuvuka vizingiti vya migogoro ndani ya nyumba kwasababu ya uwepo wa roho Mtakatifu.
7. Kutakuwepo na umoja ndani yenu kwasababu ya uwepo wa Roho wa MUNGU katikati yenu.
8. Mwenza anakuwa imara wakati wote hata kwenye majaribu kutokana na hofu ya MUNGU ndani yake.
9. MUNGU atampa ujumbe wa kukuongoza wewe kwasababu ya maombi au uchaji alio nao
10. Wewe na kizazi chako mtakuwa na ulinzi wa MUNGU muda wote
11. Wakati unatamani kuikimbia Ndoa yako,MUNGU atakurejesha kwasababu ya maombi yake.
12. Nguvu ya MUNGU ndani yenu inakuwa kubwa hata kufika ile iliomfufua Lazaro Kaburini .
13. Mtajaliwa kizazi chenye baraka zinazotoka kwa MUNGU
14. Watoto wenu pia watakuwa katika maadili ya kumpenda na kumtumikia MUNGU
15. MUNGU wetu ni pendo akiwa ndani ya Ndoa basi kunakuwa ni salama na shwari.