VIWANGO VYA SOKA KWA TIMU ZA TAIFA MWEZI HUU 2024

0:00

MICHEZO

Ivory Coast imepanda nafasi 10 duniani kwenye msimamo wa viwango vya Fifa baada ya kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika, huku Nigeria waliofika fainali wakipanda nafasi 14.

Super Eagles sasa wapo nafasi ya 28 licha ya kupoteza mchezo wa fainali, na kuwafanya timu ya tatu bora kutoka Afrika yenye viwango vya juu duniani.

Ivory Coast imesogea hadi nafasi ya 39 duniani baada ya ushindi wa Afcon.

Angola ndio wamenufaika zaidi, baada ya kupanda nafasi 24 hadi namba 93, baada ya kutinga robo fainali.

Tanzania imepanda nafasi mbili hadi 119 duniani.

Morocco imesalia kuwa timu yenye viwango vya juu Afrika, ikipanda hadi nafasi ya 12, licha ya kuondolewa kwenye 16 bora, na Senegal wapo nafasi ya 17 baaada ya kutolewa kwenye raudi hiyo ya 16.

Tunisia na Algeria zimedondoka kwa nafasi 13, na kufikia 41 na 43, baada ya kutolewa kwenye ngazi ya makundi.

Washindi wa Kömbe la Dunia 2022, Argentina wapo kileleni wakifuatiwa na Ufaransa na England.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

President Ruto Explains Why He Nominated Opposition...
President William Samoei Ruto on Thursday emphasized the need for...
Read more
𝐔𝐓𝐎𝐅𝐀𝐔𝐓𝐈 𝐖𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐍𝐀 𝐅𝐂 𝐀𝐔𝐒𝐁𝐄𝐑𝐆 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄...
Vitu vitano vinavyo itofautisha yanga na FC ausberg ni. Match fever.Kwa...
Read more
Kenyan Government Bolsters National Security as Mudavadi...
Musalia Mudavadi, the Acting Cabinet Secretary for Interior and National...
Read more
Ugonjwa wa Tezi Dume: Chanzo,Dalili na Tiba...
AFYA YA TEZI DUME KWA MWANAUME Kila mwanaume anazaliwa na Tezi...
Read more
CHIELLINI AMESTAAFU KUCHEZA MPIRA
NYOTA WETU.
See also  DRAW YA CAF, YANGA NA AZAM ZINAWEZA KUKUTANA.
Beki wa zamani wa Juventus na Timu ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply