RWANDA YAIPINGA MAREKANI KUHUSU VITA YA CONGO

0:00

HABARI KUU

Nchi ya Rwanda imeituhumu Marekani kwa kuikosoa na kupotosha ukweli kuhusu machafuko yanayoendelea Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika tangazo ambalo limetolewa na Rwanda kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nchi hiyo inaishutumu DRC kwa kuwa chanzo cha mgogoro unaoendelea baada ya Serikali ya Rais Tshisekedi kuongeza idadi ya askari jeshi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara hiyo imefahamisha kuwa imekuwa ikijaribu njia ya Kidiplomasia kuzungumza na DRC kutatua mgogoro uliopo lakini juhudi zao ziligonga mwamba.

Rwanda inasema kauli ya Marekani inapotosha ukweli, na kuongeza kuwa hatua za kutuma wanajeshi DR Congo zinatishia usalama wake na ina haki ya kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya tishio hilo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Toni Kroos atangaza kustaafu soka
MICHEZO Kiungo kutoka nchini Ujerumani na Klabu ya Real Madrid...
Read more
Changamoto ya Allergy kwa Mtoto,Dalili na Matibabu...
Changamoto ya allergy kwa watoto ni suala linalowakumba watoto wengi...
Read more
DE ZERBI ON HIS FUTURE PLANS
SPORTS De Zerbi on his future: “I’m gonna speak to...
Read more
TEMS MWANAMZIKI WA KIKE GHALI AFRIKA ...
NYOTA WETU. Tochukwu Ojogwu ,Rapa maarufu wa nchini Nigeria 🇳🇬...
Read more
ADAKWA NA POLISI KWA KUMUINGILIA KUKU NA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  SABABU DRC KUISHITAKI RWANDA MAHAKAMA KUU YA AFRIKA MASHARIKI

Leave a Reply