VLADIMIR PUTIN AMPA ZAWADI KIM JONG UN

0:00

HABARI KUU

Rais wa Urusi Vladimiri Putin amempa zawadi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un gari la kifahari lililotengenezwa Urusi.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema gari hilo liliwasilishwa kwa wasaidizi waandamizi wa Bwana Kim siku ya Jumapili.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov baadaye alithibitisha kutolewa kwa zawadi hiyo akisema gari hilo aina ya Aurus, ni la kifahari kwa hali ya juu, aina ambayo inatumiwa na Bwana Putin mwenyewe.

Urusi na Korea Kaskazini, zimeunda uhusiano wa karibu tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.

Korea kaskazini inadhaniwa kuwa inaipa Urusi silaha kwa ajili ya vita, licha ya kuwepo na vikwazo vya kimataifa dhidi ya mataifa hayo mawili, limeripoti shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC. Mataifa hayo mawili yanakanusha kuvunja kanuni za vikwazo.

Bana Putin alimualika Bwana Kim katika eneo la Mashariki la Vostochny Cosmodrome mwezi Septemba mwaka jana, ikiwa ni ziara ya kwanza ya Kim nje ya nchi katika kipindi cha miaka minne.


Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

"Envy exist in almost every extended family...
OUR STAR 🌟 Controversial Nollywood actor, Yul Edochie has taken...
Read more
Bhoeli finally changes Chelsea's transfer policy
Chelsea Football Club may abandon the idea of ​​a costly...
Read more
VIDEO YA MBOWE AKIMTUHUMU RAIS SAMIA KUIUZA...
VIDEO
Read more
'Nobody is unbeatable': Verstappen rivals believe they...
LAS VEGAS, - Max Verstappen's rivals were quick to congratulate...
Read more
RAIS KIM JONG UN AMTEMBELEA PUTIN ...
Habari Kuu Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amewasili nchini Urusi...
Read more
See also  WAFANYAKAZI POSTA WAKAMATWA KUSAFIRISHA BANGI.

Leave a Reply