MBWA WA RAIS JOE BIDEN COMMANDER NI HATARI

0:00

HABARI KUU

Mbwa wa Rais wa Marekani Joe Biden aitwaye Commander aliwang’ata maafisa usalama kwenye matukio takriban 24, nyaraka zilizotolewa zimeonesha.

Taarifa za maafisa usalama zinaonesha kiwango ambacho mbwa huyo aina ya German Shepherd alivyosababisha sekeseke kwa walinzi wa Rais.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu amesema kung’atwa huko kulisababisha maafisa usalama kubadili mbinu zao kwa “kuweka nafasi kubwa” baina ya mbwa na maafisa.

Hatua hiyo ilikuja miezi kadhaa kabla ya Commander kuondolewa Ikulu ya White House.

Nyaraka hizo zimewekwa wazi kupitia sheria ya Uhuru wa kupata habari, baada ya maombi kuwasilishwa na taarifa kuwekwa mtandaoni.

Majina ya maafisa usalama yamefichwa na hata mbinu walizotumia kujilinda.

Nyaraka zilionesha matukio yasiyopungua 24 ya kung’atwa kati ya Oktoba 2022 na Julai 2023, ikiwemo taarifa ya maafisa usalama kung’atwa mikononi, kiunoni, kifuani, mapajani na mabegani.


Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Garissa Security Forces Make Significant Arrests in...
Security personnel in Garissa achieved a significant milestone in addressing...
Read more
WANAFUNZI WAFARIKI KWA KUVUTA MOSHI WA JENERETA
HABARI KUU Wanafunzi saba wa chuo kikuu wamefariki dunia baada...
Read more
SALIM KIKEKE RASMI AJIUNGA NA EFM TANZANIA...
Habari Kuu Kwa karibu mwezi mzima ,kituo cha E kinachorusha...
Read more
Infectious Disease Expert Tapped as Kenya's New...
President William Ruto has nominated Deborah Mlongo Barasa as the...
Read more
Hot model on bikini lingerie around places
Mattis nunc sed blandit libero volutpat sed. Egestas pretium...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  AL AHLY KUIBEBA YANGA LEO USIKU? <!--INDOLEADS - END-->

Leave a Reply