MICHEZO
Uchunguzi umebaini kuwa Mwanariadha mwenye rekodi ya Dunia mbio za Marathon nchini Kenya, Kelvin Kiptum, alifariki kutokana na majeraha mabaya kichwani aliyoyapata kwenye ajali ya gari.
Maisha ya Mwanariadha huyo yalikatizwa katika ajali ya usiku wa manane karibu na nyumbani kwake Kaskazini-Magharibi mwa Kenya mnamo tarehe 11 Februari, ambapo kocha wake wa Rwanda, Gervais Hakizimana, pia alifariki.
Kifo cha Kiptum kilikuja miezi michache tu baada ya kuweka rekodi ya dunia ya saa 2 na sekunde 35 kwa wanaume katika mbio za Chicago Marathon.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 aliripotiwa kupanga kuweka rekodi za kukimbia umbali wa kilomita 42 kwa chini ya saa mbili katika mbio za marathon za Rotterdam mwezi Aprili, hatua ambayo haijawahi kufikiwa hapo awali katika mashindano ya wazi.