OMBAOMBA WAHUKUMIWA KUFUNGWA JELA

0:00

HABARI KUU

Mahakama nchini Uganda imewahukumu zaidi ya wanawake 100 kifungo cha nje cha mwezi mmoja kila mmoja huku wakitakiwa kufanya kazi za kijamii baada ya kukiri kuwatuma watoto wao kuombaomba katika Jiji la Kampala.

Mahakama pia imepiga marufuku wanawake hao kurejea katika jiji hilo na kuamuru warudishwe katika wilaya wanakotokea ya Napak, Kaskazini mwa Uganda, gazeti la Daily Monitor limeripoti.

Baada ya kukiri makosa yao, wanawake hao waliomba kuhurumiwa, huku wengine wakisema ni wajane na wengine wakisema hawana waume.

“Nimesikiliza kilio chao na kuona hukumu ya kuwatupa jela haitakuwa sawa. Lakini ni lazima nitekeleze adhabu ili kukomesha hii tabia… Nikawapa adhabu ya kufanya kazi za kijamii bila kulipwa. Watatumikia adhabu hiyo kwa mwezi mmoja,” hakimu aliyesikiliza kesi dhidi ya wanawake hao, Edgar Karakire, ameliambia Daily Monitor.

Kutuma watoto kuombaomba ni kinyume na sheria za ulinzi wa watoto za Uganda na adhabu yake inafikia hadi kifungo cha miezi sita au zaidi.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Donald Trump aongeza ushawishi kwenye majimbo mengi...
HABARI KUU Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameimarisha...
Read more
Poison that kills a man.
Once upon a time a beautiful girl got tired of...
Read more
Real Madrid forward Vinicius Jr says he...
The Brazil forward broke down in a press conference earlier...
Read more
Shooting at Donald Trump Rally
Donald Trump, the Republican presidential candidate and former U.S. president,...
Read more
SABABU YA KIFO CHA MZEE WA MJEGEJE
NYOTA WETU Msanii wa vichekesho Umar lahbedi Issa almaarufu la...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ASKOFU AJINYONGA KISA MADENI NA MGOGORO

Leave a Reply