MUHIMBILI-MLOGANZILA YAINGIZA BILIONI 8 KISA UREMBO

0:00

HABARI KUU

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imezalisha shilingi Bilioni 8 kwa kufanya tiba urembo ambapo pia wameboresha maeneo mengi ya huduma ikiwemo ununuzi wa vifaa bora na vya kisasa na kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti.

Amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ambayo imeeleza kuridhishwa na hali ya utoaji huduma katika hospitali hiyo.

“Niipongeze Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini kwani hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa ambao walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutibiwa wanatibiwa hapa nchini na tumeanza kupata wageni kutoka nje ya nchi kuja kupata huduma nchini,” ameeleza Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.

Aidha, ameitaka Serikali kupanua wigo wa utoaji huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwani hospitali hiyo bado ina eneo kubwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KOCHA JAMHURI KIWELO"JULIA" AULA SINGIDA FOUNTAIN GATE
MICHEZO Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu za Simba SC,...
Read more
TANZANIA YAKUBALI KICHAPO MBELE YA BULGARIA
MICHEZO Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza vibaya...
Read more
OUSMANE SONKO IS APPOINTED AS A SENEGAL'S...
POPULAR NEWS SENEGAL'S NEW PRESIDENT Bassirou Diomaye Faye has appointed firebrand...
Read more
Former Mandera East MP Omar Maalim's Generosity...
The residents of Mandera East constituency have expressed their heartfelt...
Read more
Sakata la Mchezaji wa Simba KIBU DENIS...
MENEJA WA KIBU ANAWADAI Simba SC Tanzania "Mchezaji (Kibu) alipomaliza mkataba,...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply