HABARI KUU
Hatimaye aliyekuwa rais wa Namibia, Hage Geingob ambaye alifariki akiwa hospitali Februari 4, 2024 wiki kadhaa baada ya kupatikana na saratani, amezikwa kwenye bustani ya mashujaa ya Heroes Acre, hapo jana siku ya Jumapili Februari 25, 2024.
Mazishi hayo yalifanyika katika viungani vya mji mkuu wa Namibia Windhoek, baada ya siku 20 za maombolezo, huku wanajeshi wakifyatua mizinga 21 kwa heshima, wakati ndege za kivita za kijeshi zikipaa angani kwenye eneo hilo.
Geingop (82), aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili na baadaye kuwa rais wa 3 wa Taifa hilo tangu lilipojipatia uhuru wake kutoka Afrika Kusini 1990, akiongoza nchi hiyo yenye watu wachache na sehemu kubwa ikiwq ni jangwa, kuanzia mwqka 2015.
Kama mmojawapo wa Wanaharakati wa uhuru, Geingop alikimbilia kwenye mataifa ya kigeni kwa miaka 27, yakiwemo Botswana, Zambia na Marekani, kabla ya kurejea nchini 1989 na aliwahi kuhudumu kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini na chama tawala cha South West African People’s Organisation – SWAPO.