MICHEZO
https://www.facebook.com/Rahman.Jahid.15/videos/7462167590508968/?mibextid=AQBXeECoIFSgMqhe
Mashabiki wa soka wamemkosoa vikali Cristiano Ronaldo baada ya kuonekana akifanya kitendo kichafu wakati wa mechi huko Saudi Arabia.
Ronaldo anayeichezea timu ya Al-Nassr alifunga bao kwa penati wakati timu yake ilipoishinda Al Shabab kwa mabao 3 -2 hapo jana.
Baada ya filimbi ya mwisho, Ronaldo alionekana akikuna sikio lake huku akirudiarudia kutembeza mkono wake mbele ya eneo la sehemu zake za siri.
Kitendo hicho kilichoeleweka kama “ishara chafu” kilionekana kuwalenga Mashabiki wa timu pinzani ambao walisikika wakiimba jina la mpinzani mkuu wa mwanasoka huyo Lionel Messi.
Kitendo hicho hakikuonyeshwa kwenye televisheni lakini kilirekodiwa na mashabiki waliokuwemo uwanjani ambao walishea video hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa gazeti la Asharq al-Awsat la Saudi, Shirikisho la soka la Saudia (SAFF) limeanza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Kupitia mtandao wa X Mwandishi maarufu nchini Saudia na Mtangazaji wa televisheni Waleed Al Farraj ,amesema “Kamati ya Nidhamu inakabiliwa na mtihani mkubwa, tutangojea, tuone”
“Kila kitu kina mipaka yake, haijalishi una umaarufu kiasi gani. Hivi ndivyo Ligi kubwa zilivyo.”
Hii si mara ya kwanza kwa mwanasoka huyo kukosolewa kwa vitendo kama hivi.