UFAHAMU MSIKITI MKUBWA ZAIDI BARANI AFRIKA

0:00

HABARI KUU

Rais wa Algeria Abdelmajid Tebbourne siku ya Jumapili alizindua Msikiti Mkuu wa Algiers, ambao ni msikiti mkubwa zaidi barani Afrika.

Msikiti huu ni wa tatu kwa ukubwa duniani, nyuma ya misikiti miwili iliyopo Maka na Madina.

Msikiti huo umejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 70 na unaweza kuchukua waumini 120,000.

Msikiti huu pia una mnara mrefu zaidi duniani.

Unatarajiwa kutumiwa wakati wa mwezi wa Ramadhan unaoanza wiki mbili zijazo.

Msikiti huu ulijengwa kwa muda wa miaka saba na kugharimu zaidi ya dola milioni 800.

Ujenzi wa msikiti huu ulikuwa mradi wa Rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ambaye aliondoka madarakani baada ya nia yake ya kutaka kuwania urais kwa muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.


Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

DANNY DRINKWATER AKUBALI YAISHE ...
NYOTA WETU Kiungo wa zamani wa Manchester United, Leicester City...
Read more
BOBRISKY FAILS TO MEET BAIL CONDITIONS ...
OUR STAR 🌟 Popular crossdresser Bobrisky has reportedly failed to...
Read more
Tume ya Haki Za Binadamu Yamsafirisha PAULINE...
Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora...
Read more
MAJALIWA ATAKA MWAROBAINI WA NDOA NCHINI ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MASTAA WA BONGO WALIOZAA, KUACHANA NA WENZA...
MASTORI Listi ya mastaa wa Bongo ambao wamejaaliwa kupata watoto...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MACKY SALL KUONDOKA MADARAKANI

Leave a Reply