MAURICIO POCHETTINO APONGEZWA NA WAMILIKI WA CHELSEA

0:00

MICHEZO

Meneja wa Chelsea Mauricio Pochettino amesema wamiliki wa klabu hiyo wameonesha kumuunga mkono tangu alipopoteza mchezo wa fainali ya Carabao dhidi ya Liverpool.

Pochettino alishutumiwa na mashabiki na hata wachambuzi baada ya Chelsea kufungwa 1-0 na Liverpool dhaifu siku ya Jumapili.

Alisema amekuwa na mazungumzo chanya na wamiliki Todd Boehly na Behdad Eghbali.

“Wameonesha kuniunga mkono na baada ya mchezo Todd alinitumia ujumbe mzuri tu,” alisema Pochettino.

“Nilisalimiana nao nilipowaona uwanjani na baadaye nilikutana na Behdad na tukazungumza.

“Tulizungumza kuhusu mchezo na nafasi tuliyopoteza ya kushinda kombe, kwa sababu nadhani tulicheza vizuri katika dakika 90.”

Alipoulizwa kuhusu hatma yake Chelsea, Pochettino alisema: “Sio juu yangu. Tuna uhusiano mzuri sana na wamiliki na mkurugenzi wa michezo.

“Ni juu yao kuniamini au kutoniamini. Sio uamuzi wa kocha.”


Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Adam Peaty has tested positive for Covid-19...
Peaty missed out on a third consecutive gold medal by...
Read more
KATIBU MKUU CCM NCHIMBI AWATISHA VIONGOZI WAZEMBE...
HABARI KUU KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi...
Read more
Forward Steve Bergwijn was not considered for...
Bergwijn, 26, signed for Al-Ittihad from Ajax for £17.7m on...
Read more
YUL EDOCHIE CELEBRATES DAUGHTER, DANIELLE ON HER...
CELEBRITIES Controversial actor, Yul Edochie causes a buzz online as...
Read more
Al Ahly Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa...
Rasmi, Klabu ya Al-Ahly ya Misri imetawazwa kuwa bingwa wa...
Read more
See also  HERSI SAID ALAMBA SHAVU CAF

Leave a Reply