WAZIRI MKUU ETHIOPIA KUZURU TANZANIA

0:00

HABARI KUU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Dkt. Abiy Ahmed Ali anatarajiwa kuwasili Nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kuanzia February 29 hadi March 02, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema Dkt. Abiy atapokelewa rasmi Ikulu, Dar es salaam March 01, 2024 na Mwenyeji wake Rais Samia.

Lengo la ziara hii mbali na kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Nchi hizi mbili, inalenga pia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Ethiopia ambazo zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya biashara na uwekezaji, elimu, utamaduni, usafirishaji wa anga, kilimo, mifugo, udhibiti wa uhamiaji holela, ulinzi na usalama.

Tanzania na Ethiopia zina uhusiano wa kidiplomasia wa muda mrefu na wa kihistoria ambao ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtawala wa Ethiopia, Hayati Haile Selassie, Viongozi hawa walishirikiana bega kwa bega katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na ni miongoni mwa Viongozi Waanzilishi 32 wa Umoja wa Afrika wakati huo OAU mwaka 1963.

Aidha, mbali na ushirikiano wa kidiplomasia, Tanzania na Ethiopia zinashirikiana katika sekta ya anga ambapo mwaka 2016 hadi 2023 jumla ya marubani 75 na wahandisi 25 kutoka Tanzania wamepokea mafunzo katika ngazi tofauti nchini Ethiopia, hivyo ni wazi kuwa, ziara hii itafungua milango zaidi ya ushirikiano kati ya Shirika la Ndege la Ethiopia na Shirika la Ndege la Tanzania – ATCL katika kujiendesha kibiashara.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  Wanaomtusi TUNDU LISSU waonywa

Related Posts 📫

ROMANTIC THINGS TO DO THAT DON'T INVOLVE...
LOVE TIPS ❤ When romance is often mentioned, many think...
Read more
MDEE NA WENZAKE BADO BADO CHADEMA
HABARI KUU Mahakama kuu imetengua uamuzi wa Baraza Kuu La...
Read more
SABABU ZINAZOPELEKEA KUJAMBA UKENI
AFYA Hili ni tatizo linalowakumba WANAWAKE wengi sana tena sana...
Read more
16 ADMIRABLE ATTITUDES THAT MAN FALL IN...
LOVE ❤ If you don't want to grow white hairs...
Read more
John Cena announces he will be retiring...
WWE legend John Cena has revealed when he will be...
Read more

Leave a Reply