AFIA GESTI AKIWA NA MPENZI WAKE

0:00

HABARI KUU



Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahamudu Mbwana, miaka 44, Mkazi wa Mbezi Madale, jijini Dar es Salaam, amefariki dunia akiwa na mpenzi wake, kwenye nyumba ya kulala wageni Ya Another Coast, maeneo ya Mikumbi, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, ACP Andrew Ngassa, amesema, baada ya mpenzi wake huyo kuhojiwa na polisi, alisema tarehe 26/2/2024, majira ya saa kumi alfajiri marehemu alianza kuishiwa nguvu na kuanza kukoroma.

Polisi baada ya kupata taarifa walifika eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu, na walipopekuwa nguo zake walikuta dawa ya kulevya aina ya bangi kwenye mfuko wake wa suruali.

Marehemu alikuwa anafanyakazi kwenye kampuni ya Lujuni Costruction Limited, inayojishughulisha na ujenzi wa barabara, na tayari mwili marehemu umekabidhiwa kwa mwajiri wake.
Jeshi la polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa mahojiano zaidi.


Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

7 AGREEMENTS YOU MUST DO BEFORE YOUR...
FINANCIAL AGREEMENT. You need to agree on mode of communication and...
Read more
HISTORIA YA MADILU SYSTEM
Amezaliwa:28 Mei 1952 Amekufa:11 Agosti 2007 Jean de Dieu Makiese kama...
Read more
Guinea stadium crush kills 56 people after...
CONAKRY, - A controversial refereeing decision sparked violence and a...
Read more
YANGA NA SIMBA VITANI LIGI YA MABINGWA...
Magazeti Karibu Mtanzania kwenye mbao za magazeti ya hivi leo...
Read more
HOW TO SEDUCE A PRETTY GIRL
❤ 1. Kissing is not just meant for sex.2. You...
Read more
See also  Vladimir Putin amezionya nchi za Magharibi kuacha mpango wa kuipa Ukraine Silaha za kuishambulia Urusi

Leave a Reply