GHANA YAJIPANGA KUWAKABILI WANAOJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA

0:00

HABARI KUU

Bunge la Ghana limepitisha Muswada mkali dhidi ya watu wanaojitambulisha kwa jinsia na mahusiano yasiyokubalika kisheria.

Chini ya muswada huo, mtu yeyote atakayekutwa na hatia hiyo atahukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela.

Aidha, watakaoanzisha au kuyafadhili makundi ya watu wa aina hiyo watahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Pamoja na hayo, wale wote watakaohusika na kuhamasisha tabia na vitendo hivyo wakilenga watoto watahukumiwa kifungo cha miaka kumi jela.

Muswada huo pia umehimiza wananchi kuwaripoti kwa Mamlaka wale wote wanaojihusisha na tabia na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Muswada huo ulioungwa mkono na vyama vikubwa viwili vya nchini humo, utaanza kutumika ikiwa Rais Nana Akufo-Adoo atatia saini na kuufanya kuwa sheria.

Rais Akufo-Addo alikwisha ahidi ya kuwa yupo tayari kutia saini muswada huo ikiwa Waghana walio wengi watamtaka kufanya hivyo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Timaya calls out member of his team...
CELEBRITIES Popular musician, Timaya extensively berates a member of his...
Read more
Hoja nane za ACT-WAZALENDO kwenda kwa Rais...
"Matukio ya vitisho, ukamataji, kupigwa, kuteswa na kuumizwa kwa wanachama...
Read more
16 QUALIFICATIONS OF BEING A HEAD OF...
LOVE TIPS ❤ Many men love to lay claim of...
Read more
After Spain’s triumph over England in the...
Spain emerged victorious with a 2-1 win over England on...
Read more
12 REASONS WHY YOU SHOULD AVOID PREMARITAL...
❤ 1. Premarital sex produces extramarital sex. Those who sow...
Read more
See also  MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFIA MADARAKANI

Leave a Reply