MAPENZI
1. KUPUNGUA KWA MAWASILIANO.
Mwenza wako huwa anakosa muda wa kuwasiliana na wewe kwenye mazungumzo ya kawaida na hata akijilazimisha basi yatakuwa tu ni mambo ya kawaida.
2. KUKOSEKANA KWA UKARIBU.
Kihisia na kimwonekano huwa kunapungua hasa ukimtazama na kumuwaza mwenza wako. Katika mazingira haya,huwezi kumbusu wala kumkumbatia mwenza wako.
3. MASWALI KWENYE MAONGEZI.
Mtu ambaye huna hisia nae huwa ni ngumu kuwa na hisia chanya ambazo zinaweza kuzalisha maneno yenye faraja na furaha . Mara nyingi; Mawasiliano yatakuwa ya maneno,hisia za mwili ambazo ni za maulizo sana.
4. KUKOSEKANA KWA BIDII NA MVUTO.
Mtu ambaye anakosa mvuto kwako hawezi kuwekeza kwaajili ya maisha yenu ya baadaye hata bidii ya kutafuta haiwezi kuwa ya kivile kwasababu haupo kwenye mipango yake.
5. KUKOSEKANA KWA HISIA.
Pale ambako hutaki kumuona wala kusikia sauti yake ,ni dalili tosha kwamba huwezi kuendelea nae hatua zaidi ya kimaisha.