ARIEL HENRY AJIUZULU KUWA WAZIRI MKUU WA HAITI

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa Taifa la Caribbean, Kiongozi wa jumuiya ya kikanda na Rais wa Guyana, Irfaan Ali ametangaza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry (74), ambaye amekuwa akishililia nafasi hiyo isiyo ya kuchaguliwa, tangu mauaji ya mwaka 2021 ya Rais wa mwisho wa nchi hiyo, Jovenel Moise.

Kujiuzulu kwa Henry, kunajiri baada ya Viongozi wa eneo hilo kukutana katika nchi jirani la Jamaica kujadili mfumo wa mpito wa kisiasa, ambao Marekani ilitaka uharakishwe, huku magenge yenye silaha yakitaka kupindua serikali yake.

Henry, ambaye raia wengi wa Haiti wanamchukulia kuwa fisadi, alikuwa ameahirisha uchaguzi mara kwa mara akisema lazima usalama urejeshwe kwanza ambapo muhula wa mwisho wa Maseneta wa Haiti ulimalizika mwanzoni mwa mwaka 2023.

Haiti ilitangaza hali ya hatari mwezi huu (Machi), huku mapigano yakiharibu mawasiliano na kupelekea wafungwa kutoroka mara mbili Gerezani baada ya Kiongozi wa muungano wa makundi yenye silaha, Jimmy “Barbeque” Cherizier kusema wangeungana na kumpindua Henry.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KATUMBI NA TSHISEKEDI NANI KUICHUKUA DRC?
HABARI KUU Jumla ya wagombea wanne wa urais nchini CONGO...
Read more
MAGAZETI YA LEO 29 MEI 2024
Read more
MFAHAMU MWANAUME MWENYE MVUTO ZAIDI DUNIANI
NYOTA WETU Muigizaji mtanashati kutoka Marekani Michael B Jordan amefunguka...
Read more
DREAMLINER YA ATCL YAKWAMA MALAYSIA KWA MIEZI...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Borno South Senator, Ali Ndume on Tuesday...
Ndume said the new office does not reflect his seniority...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  RAIS WA HUNGARY AJIUZULU WADHIFA WAKE

Leave a Reply