SABABU ZA MGOMO WA MADAKTARI KENYA

0:00

HABARI KUU

Mgomo wa madaktari katika Hospitali za Umma kote Nchini Kenya, umeanza rasmi hii leo Machi 14, 2024, huku baadhi ya jamaa wakilazimika kuwaondoa wagonjwa wao katika Hospitali hizo, ili kutafuta huduma za matibabu kwingine.

Hata hivyo, shughuli za kawaida katika Hospitali kuu ya Rufaa na Mafunzo ya Kilifi zimeendelea, hivyo kukinzana na tamko la Muungano wa Madaktari ukanda wa Pwani – KMPDU, la mgomo wa Madaktari.

Mmoja wa wauguzi aliyeongea kwa sharti la kutotaja jina, amesema wanaendelea na kazi ya kuhudumia wagonjwa kama kawaida, baada ya uongozi wa madaktari Kilifi kufanya mkutano na Serikali ya Kaunti ya Kilifi.

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya – KPMDU, ulitangaza mgomo wakiishinikiza Serikali kutimiza mahitaji yao muhimu, ikiwemo kurejeshwa kwa makato ya ushuru wa Nyumba yaliyofanyika katika mishahara yao, ambayo Mahakama ilitangaza kuwa yanafanyika kinyume na Katiba.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WHAT YOU NEED TO KNOW ABOUT KISSING...
❤ 1. Kissing is not just meant for sex2. You...
Read more
Manchester City claim victory in legal challenge...
Manchester City claimed a partial victory over the Premier League...
Read more
HENNOCK INONGA TAYARI KASAJILIWA NA TIMU HII
MICHEZO Beki wa kati wa klabu ya Simba SC, Hennock...
Read more
STEPS THAT WILL HELP TO BUILD UP...
❤ WHAT EXACTLY IS AN ORGASMOrgasm can be defined...
Read more
SABABU GAMONDI KUMPIKU BENCHIKHA KWENYE TUZO
NYOTA WETU/MICHEZO Kocha Miguel Gamondi wa Yanga SC amechaguliwa kuwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  WATU ZAIDI YA 100000 WALIVYOKIMBIA VITA DRC

Leave a Reply