HABARI KUU
Wakati leo Alhamisi Machi 14, 2024 ikiwa ndio mwisho wa kuondoa kwa hiari namba zilizoongezwa ukubwa ‘3D’ kwenye magari, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani, limeainisha hatua zitakazochukuliwa kwa mtu ambaye gari lake litabainika kuendelea kutumia namba hizo zilizopigwa marufuku.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, Kamanda Ramadhani Nga’nzi, amesisitiza muda wa wiki mbili walioutoa kwa watu kuondoa 3D kwa hiari unaisha leo, hivyo kuanzia kesho Ijumaa Machi 15, wataanza msako utakaohusisha watengenezaji na wanaoendelea kukaidi kuziweka.
Kamanda Nga’nzi amesema miongoni mwa hatua watakazozichukua ni kupiga faini, kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watakaobainika kuendelea kuzitengeneza na watumiaji.
Februari mwaka huu, jeshi hilo lilipiga marufuku matumizi ya namba 3D katika magari kwa sababu sio namna rasmi katika nchi ya Tanzania, badala yake lilielekeza wamiliki wa magari kutumia namba za 2D zilizoidhinishwa na msajili wa magari kupitia mawakala.
Sababu nyingine ya kupiga marufuku 3D ni kwamba namba hizo haziko kwenye mfumo wa Tanzania, kwa kuwa hazina ubora unaotakiwa, zinatengenezwa na watu wasioidhinishwa kuwa mawakala wa namba za magari.
Akizungumza leo Alhamisi Machi 14, 2024 Kamanda Nga’nzi amesema, “Tukiwakuta wameweka namba za 3D tutaziondoa na kuwataka kuweka namba 2D au kuwaandikia faini ya Sh30,000 makosa ya papo kwa papo kwa kutembea na namba zisizoruhusiwa.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.