Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar.

0:00

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe huku aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya akihamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Martin Otieno aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  RAIS SAMIA SULUHU KUWALINDA CHADEMA
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading