BONDIA WA KWANZA WA TANZANIA AONDOLEWA KWENYE ALL AFRICAN GAMES

0:00

MICHEZO

Ajali ya kuvunjika mkono katika raundi ya mwisho ya mchezo imemuondoa katika mashindano bondia Abdallah Abdallah “Katoto” aliyekuwa akipambana na Wibshet Bekele kutoka Ethiopia.

Ilikuwa katika bout no. 3 ya hatua ya 16 bora ya mashindano hayo katika uzani wa Fly weight 51kg ambapo Katoto alipata ajali hiyo akijiandaa kufanya shambulizi dhidi ya mpinzani wake katika raundi ya 3 na ya mwisho ambapo alipata ajali hio na kumlazimu mwamuzi wa mchezo kusimamisha pambano na Katoto kupelekwa moja kwa moja hospital kwa ajili ya matibabu.

“Katoto tulimwahisha kwenda University of Ghana Medical Center kwa ajili ya matibabu na baada ya kuchukuliwa vipimo alionekana amevunjika sehemu ya katikati ya mkono, ila tunashukuru Mungu hali yake binafsi inaendelea vizuri ingawa hatoweza kucheza kwa kipindi cha karibuni” alisema Muhsini Mng’ola, Mwalimu Msaidizi wa timu ya Taifa ya ngumi.

Baada ya pambano hilo Katoto alikuwa apambane hatua ya robo fainali dhidi ya Patrick Chinyemba kutoka Zambia ambaye ni Bingwa wa Afrika na tayari ameshakata tiketi ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024.

“Ndoto yangu kubwa sana ilikuwa katika pambano langu la robo fainali dhidi ya Chinyemba wa Zambia na kutaka kuishangaza Afrika na Dunia kwa uwezo wangu, pambano hili la Muethiopia nilikuwa na uhakika na ushindi kwa maandalizi mazuri tuliyoyapata” alisema Katoto.

Bondia huyo machachari kama kawaida yake alikuwa ameshajizolea idadi kubwa ya mashabiki katika ukumbi wa Bukom Arena kwa aina ya uchezaji wake wenye mvuto mkubwa kwa mashabiki.

Naye Raisi wa Shirikisho Ndg Lukelo Willilo alisema “Tunamshukuru Mungu kwa yote, ndio mchezo ulivyo, zilikuwa zimebaki sekunde chache pambano liishe huku tukiongoza kwa matokeo, lakini mchezo wakati mwingine una matokeo katili”

See also  Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imekamilika huku vigogo 8 waliofuzu hatua hiyo wakibaini wapinzani wao.Kama kawaida, Washika Mitutu, Arsenal wamepangwa dhidi ya Bayern Munich kwenye hatua hiyo huku Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo, Manchester City wakikutanishwa na Mabingwa wa kihistoria, Real Madrid.Barcelona imepewa PSG huku Atletico Madrid ikipewa Borussia Dortmund.DROO KAMILI Arsenal 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 vs. 🇩🇪 Bayern MunichAtletico Madrid 🇪🇸 vs. 🇩🇪 DortmundReal Madrid 🇪🇸 vs. 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Manchester CityParis Saint-Germain 🇫🇷 vs. 🇪🇸 BarcelonaMshindi kati ya Arsenal na Bayern Munich atachuana na mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City kwenye hatua ya nusu fainali.Mshindi kati ya PSG na Barcelona atachuana na mshindi kati ya Atletico Madrid dhidi ya Borussia Dortmund.

Wakati huo huo, session ya 2 ya mapambano ya jana ilihairishwa mpaka leo jioni ambapo bondia Abdallah Mfaume “Nachoka” alikuwa apambane na Gerald Kabinda kutoka Zambia katika hatua ya 16 bora uzani wa Welterweight.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading