HABARI KUU
Mzozo umeibuka katika mitandao ya kijami nchini Tanzania baada ya serikali ya Marekani kwa ushirikiano na jumuiya za kimataifa kutoa msaada wa chakula kwa shule zilizopo mjini Dodoma.
Msaada huo unashirikisha mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani
Kulingana na Marekani mpango huo unaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni.
Hatahivyo hatua hiyo haikupokelewa vyema na watumiaji wa mitandao nchi humo waliohoji iwapo taifa hilo linahitaji msaada wa chakula
Elias G balimponyakatika mtandao wake wa X alihoji: Hivi Tanzania tunahitaji msaa wa chakula kweli? Aliongezea: Chakula??? MAHARAGWE, MCHELE, MAFUTA YA ALIZETI??
Alisema: Ndugu zangu Marekani njooni tushirikiane katika mambo mengine muhimu ya kuinua uchumi. Tanzania kusaidiwa chakula HAPANA . Natamani kumfahamu kiongozi wangu aliyeomba msaada wa CHAKULA. Jamaa huyo badala yake aliitaka Marekani kutoa misaada kama hiyo kwa taifa la Sudan
Kwa upande mwengine mtumiaji mwengine wa mtandao wa X kwa jina CAT POWER alishutumu hatua hiyo akitaka waziri aliyepokea msaada huo kufutwa kazi mara moja..
Alisema kwamba Tanzania ni mlimaji mkubwa wa mchelele wa kutosha hadi unakosa soko. Alihoji ni vipi watumie mchele wenye virutubishi kutoka Marekani?.
Mtumiaji mwengine wa mtandao wa X kwa jina Lings, aliuliza maswali kadhaa. Je tumefika huku? Ni kweli tuliomba hiki chakula? Je tunakufa njaa? Hatuwezi kulisha watoto wetu? Mchele? Kweli Mchele? Kwanini wasipeleke nchi zenye njaa?
Aliendelea kusema: Nina hakika kwamba hatukuomba wala hatuhitaji, Wanatupa michele?
Mwengine kwa jina Yoab Mwana wa Seruya alisema: Tunashukuru lakini, HAPANA hatuhitaji huu mchele. Alisema Mchele wetu wa Mbeya upo wa kutosha sana. Alitaka msaada huo wa chakula kupelekwa katika kambi za wakimbizii huko Kigoma .
Aliongezea: Au pelekeni Sudan Kusini .Sisi Hatuutaki. Taifa letu linajitosheleza kwa Chakula alihitimisha.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.