Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini – TMA, imetoa angalizo kwa wakazi wanaoishi ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba kuna uwezekano wa kukutana na hali mbaya ya hewa kwa siku tano na Mvua za siku tatu mfululizo.

0:00

Kupitia utabiri wake wa hali ya hewa, TMA imeeleza kuwa, maeneo mengine yanatakayokumbwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imeeleza kuwa, hali hiyo itakayosababisha mvua kubwa itaendelea hadi Machi 21, 2024 huku ikisema, “zingatieni na jiandaeni. Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.”

Februari Mosi, 2024, TMA ilitoa utabiri wake ikieleza kwamba bado kuna viashiria vya mvua za El Nino hadi Aprili 2024, kwa maeneo yanayopata mvua kwa msimu mmoja.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

CHADEMA YAMTOSA MATIKO UBUNGE TARIME MJINI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
KOSA LA JK HILI KWA LOWASSA ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Gavi delighted to be back after 348-days...
Barcelona midfielder Gavi said on Sunday he was thrilled to...
Read more
Kwanini Mwanaume Aliyemuua Mke Wake Amekataa Kupimwa...
MFANYABIASHARA Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na...
Read more
Eric ten Hag admitted that Brentford win...
While Manchester United's 2-1 victory over Brentford was their first...
Read more
See also  KIONGOZI MKUU WA AL-SHABAAB AUAWA

Leave a Reply