MICHEZO
Ofisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe amewataka wananchi kutohofia majeraha yanayowakabili wachezaji wao badala yake wajipange kujitokeza Kwa wingi katika mchezo wao wa robo fainal ligi ya mabingwa Afrika mwisho wa mwezi huu dhidi ya Mamelod Sundown.
“Wote tuliona namna wachezaji wetu wawili walivyoshindwa kuendelea na mchezo hapo jana Pacome alilazimika kutoka nje kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata dhidi ya Azam na Yao pia alipata maumivu ya paja
Daktari amesema ripoti kamili itatoka baada ya saa 72 Kwa maana ya kesho jioni ndiyo tutajua hali halisi ya wachezaji hao baada ya vipimo kukamilika
Lakini wachezaji wengine ambao wapo majeruhi ni Khalid Aucho naye daktari amesema wiki ijayo ataanza mazoezi ya mpira, Kibwana Shomari na Zawadi Mauya nao wanaendelea na Matibabu
Niwaaambie wananchi mechi dhidi ya Mamelod si mechi ya Pacome Wala mechi ya Aucho ni mechi ya mashabiki hivyo nawaomba mje Kwa wingi tumalize shughuli Benjamin Mkapa kama tulivyofanya dhidi ya CR Belouizdad” Ally Kamwe Meneja wa Habari na mawasiliano Yanga SC.