HABARI KUU
Waangalizi kutoka Burundi wamesema Uchaguzi wa Urusi ambao umempatia Rais Vladimir Putin kuongoza muhula wa tano mfululizo, ulikuwa huru na haki.
Kwa mujibu wa Prosper Ntahorwamiye aliyekuwa anaongoza kundi la waangalizi kutoka Burundi katika uchaguzi huo, amefahamisha kuwa raia walichagua wakiwa katika hali ya utulivu bila ya kuwa na usumbufu wowote baadhi ya wapiga kura wakitumia njia ya kisasa katika kumchagua Rais wao.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umeukosoa uchaguzi huo kuwa haukuwa huru na haki kutokana na baadhi ya wapiga kura kuuawa na kukamatwa.
Rais Vladimir Putin ameshinda uchaguzi ambao utamuweka madarakani hadi mwaka wa 2030.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.