SUA YAPONGEZWA KWA MATUMIZI YA BILIONI 74 VIZURI

0:00

HABARI KUU

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) kimepokea jumla ya shilingi bilioni 73.6 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa HEET.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Raphael Chibunda amesema fedha hizo zimetumika katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na  upanuzi wa miundombinu, mapitio ya mitaala, ununuzi wa vifaa vya kuboresha maabara, karakana, na mashamba ya mafunzo, pamoja na kuongeza ushirikiano na Mataifa mengine.

Amesema, wamesaini  makubaliano na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kuwapata wataalamu wa kilimo wenye sifa kwa miradi mbalimbali, na kwa sasa vijana 300 wanafanya kazi ya Maafisa Ugani katika Mikoa mbalimbali Nchini.

“Kwasbabu tumeingia makubaliano na wizara ya kilimo na kuna mambo ambayo tumeyaainisha na kuyabaonisha ambayo yatakuwa majukumu ya chuo cha kilimo moja wapo kama nilivyosema mwanzo sisi tunawasaidia kwenye kutafuta,kuchuja vijana ambao tunaamini wanaweza kuwa sehemu ya huo mradi,” amesema Chibunda.

Hata hivyo,  SUA inajivunia Mafanikio makubwa ya ongezeko la idadi ya Wanafunzi Chuoni, ambapo katika miaka mitatu iliyopita kumekuwa na ongezeko la zaidi ya Wanafunzi 3800 kutoka nchini na baadhi yao kutoka mataifa mengine Duniani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ALIOU CISSÉ KOCHA MKUU SENEGAL 2026
MICHEZO Kocha wa timu ya Taifa ya kandanda ya Senegal,...
Read more
ISRAEL YASHITAKIWA MAHAKAMA KUU YA UMOJA WA...
HABARI KUU Mahakama Kuu ya Umoja wa Mataifa leo Jumatatu...
Read more
BONDIA MTANZANIA DULLA MBABE APIGWA KWA KNOCK...
MICHEZO
See also  MAWAZIRI WA SADC WAIPA TANZANIA MKONO WA POLE
Bondia Mtanzania Abdallah Pazi almaarufu Dulla MBABE amepigwa kwa...
Read more
Emilio Nsue López atangaza kurejea kwenye soka
MICHEZO Kinara wa ufungaji kwenye Fainali za Mataifa ya Bara...
Read more
Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kiume
AFYA Kumekuwa na imani nyingi kuhusu dalili za mimba ya mtoto...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply