PROFESA JANABI ATOA SIRI YA KILICHOBAINIKA KWA WATOTO WENYE UZITO ULIOPITILIZA

0:00

MASTORI

Siku mbili baada ya watoto waliokuwa na uzito kupita kiasi, Imani na Gloria Joseph kuruhusiwa kutoka hospitalini, kilichobainika chatajwa, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ikiingia katika hatua ya pili ya uchunguzi.

Hayo yamesemwa jana Alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi wakati wa mahojiano na vyombo vya habari.

Amesema baada ya kuwapima vipimo mbalimbali vya mafuta, moyo, figo, kisukari na vipimo vingine vikubwa kama CT Scan, MRI na vinginevyo watoto hao hawajabainika kuwa na tatizo lolote laa kiafya.

“Tunakwenda hatua ya pili kwa sababu hawa wote wanapimwa kupitia gharama za Serikali hakuna wanacholipa….mwisho lazima kujua ni jeni gani ambayo imeleta hitilafu kubwa namna hii kwa mtoto wa miaka mitano kuwa na uzito wa kilo 61. Ni tatizo ambalo tunalifanyia uchunguzi, tukiweza kugundua kwanza itatusaidia kuelimisha hospitali na taasisi nyingine, wazazi, ndugu na jamiii kwa ujumla,” amesema Profesa Janabi.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

AZIZ KI NA YANGA MAMBO YAKO HIVI
NYOTA WETU. Taarifa zilizopo ni kuwa Klabu ya Yanga ya...
Read more
SEAN PAUL HUU 2023 UMEKUWA MWAKA WAKE...
NYOTA WETU Msanii wa Dancehall , Sean Paul ameongoza kwenye...
Read more
9 SEX YOU MUST NEVER HAVE IN...
Sex is lawful in marriage, it’s one of the rights...
Read more
Roberto De Zerbi kuiacha Brighton
MICHEZO Kocha wa klabu ya Brighton ya Ligi kuu...
Read more
Mambo Usiyoyajua Kuhusu chura
USIYOYAJUA KUHUSU CHURA HAYA HAPA Chura ni miongoni mwa viumbe wasipendwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply