JINSI SERIKALI YA TANZANIA INAVYOTUMIA MABILIONI KWAAJILI YA TIMU ZA TAIFA

0:00

MAKALA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 Wizara kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 2.4 kugharamia Timu mbalimbali za Taifa katika mashindano ndani na nje ya nchi.

Mhe. Ndumbaro amesema hayo wakati akiwasilisha utekekezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2023/24 na Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 24/25 kwenye Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo leo Machi 22, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.

Amezitaja baadhi ya timu hizo kuwa ni Timu ya Taifa ya ya Gofu Wanawake iliyoshiriki mashindano ya Gofu Afrika Mashariki na Kati nchini Rwanda mwezi Novemba na kuwa mshindi wa kwanza, Timu ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) ambayo iliwezeshwa kushiriki michuano ya kufuzu kucheza WAFCON yanayotarajiwa kufanyika Juni, 2024 nchini Morocco, kuwezesha Timu nane ikiwemo Judo, Riadha, Mpira wa Miguu Wanawake, ngumi kriketi wanaume na Wanawake kushindana mashindano ya Michezo Afrika (All African Games) yanayoendelea nchini Ghana ambapo hadi sasa medali mbili za mchezo wa ngumi zimepatikana.

Mafaniko mengine ambayo ameyataja Mhe. Waziri ni kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambapo hadi Februari 2024, Wizara kwa kushirikiana na Benki za CRDB na NBC imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.2 kwa miradi 216 katika Halmashauri 31 za mikoa 16 ya Tanzania Bara.



“Kwa kipindi cha mwezi Julai 2023 hadi Februari 2024 Wizara imetumia takriban Bilioni 10.17 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa eneo changamani la michezo, ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa,ujenzi wa vituo vya mazoezi na kupumzikia Dodoma na Dar es Salaam na ujenzi hosteli za Chuo Cha Michezo Malya ambao unaendelea” amesema Mhe. Ndumbaro.

See also  WAFAHAMU WAKUU WA MAJESHI TANZANIA 1964 MPAKA 2023



Katika Mpango wa Bajeti ujao Mhe. Ndumbaro ameeleza kuwa, Wizara pamoja na Taasisi zake imepanga kutekeleza miradi 15 yenye thamani ya Bilioni 258 ikiwemo ujenzi wa ukumbi wa wazi wa Sanaa, Ukarabati wa Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ujenzi wa Akademia ya Michezo Malya, ujenzi wa eneo changamani la michezo Dodoma na jumba changamani la filamu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko ameipongeza wizara kwa namna ilivyotekeleza majukumu yake vyema kwa kipindi hicho, huku akisistiza kukamilika kwa wakati ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa pamoja na kutekeleza vyema Mkakati wa ubidhaishaji lugha ya Kiswahili.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

YANGA KUIKOSA HUDUMA YA LOMALISA ...
MICHEZO. Beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa ataukosa mchezo...
Read more
New Zealand coach lauds Ravindra, O'Rourke for...
BENGALURU, - New Zealand coach Gary Stead said all-rounder Rachin...
Read more
SABABU TFF KURUDISHA LIGI YA MUUNGANO
MICHEZO Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20 Kombe...
Read more
SIR FERGUSON AFIWA NA MKEWE ...
Michezo Meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson...
Read more
MAMBO 13 AMBAYO NI ALAMA KWA EDWARD...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply