BUNGE LA TANZANIA LAKANUSHA MADAI YA MBOWE KUHUSU MISHAHARA MIPYA YA WABUNGE

0:00

HABARI KUU

Bunge la Tanzania limekanusha madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ambapo alidai kwamba mishahara ya Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=) hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)

Madai hayo aliyetoa jana ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara

Taarifa ya Bunge imeeleza kuwa taarifa hizo ni uzushi na kueleza kuwa hakuna mbunge aliyeongezewa mshahara na nyongeza ya mishahara ni suala linalozingatia bajeti

“Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi na upotoshaji kwa kuwa hakuna Mbunge aliyeongezewa mshahara kama alivyodai. Hivyo, tunapenda kuwashauri na kuwasihi wananchi kupuuza madal hayo ambayo lengo lake ni kuleta taharuki pamoja na kuwagombanisha wananchi na wawakilishi wao”

“Nyongeza ya mshahara ni suala linalozingatia bajeti na hakuna utaratibu wa aina yoyote kama huo ambao umefanyika kwa ajili ya kuwaongezea Waheshimiwa Wabunge mishahara” imeeleza taarifa hiyo ya bunge .

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

UMEME WAMWIBUA MWITA WAITARA
HABARI KUU Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara...
Read more
MAKONDA ATOA MBINU HIZI KUONGEZA KASI YA...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametoa muda wa...
Read more
NCHIMBI AMTAJA SAMIA KUONGOZA KWA DEMOKRASIA
HABARI KUU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM,...
Read more
Chelsea kumuuza Trevoh Chalobah
MICHEZO Klabu ya Chelsea iko tayari kumuuza Trevoh Chalobah kwa...
Read more
MUIGIZAJI WA NOLLYWOOD AMAECHI MUONAGOR AFARIKI DUNIA...
NYOTA WETU Muigizaji Mkongwe wa Nollywood Nigeria, Amaechi Muonagor amefariki Dunia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  SPIKA WA BUNGE ANASURIKA KULALA JELA

Leave a Reply